Alhamisi 12 Machi 2026 - 14:25
Siku ya Quds ya Mwaka Huu Igeuke Kuwa Jukwaa Kubwa la Kihistoria

Hawza/ Mkuu wa Hawza nchini Iran, amesisitiza kuwa Siku ya Quds ya mwaka huu ni tofauti na miaka mingine, kwani inakuja katika kipindi muhimu na cha mabadiliko makubwa ya kihistoria nchini Iran, katika eneo la Mashariki ya Kati na duniani kwa ujumla, sambamba na vita ya Ramadhani inayoamua hatima ya mambo.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Alireza Arafi, Mkuu wa Hawza za Elimu ya Dini, ametoa taarifa maalumu akiwahimiza wananchi wa Iran, wanaoshikamana na Mapinduzi ya Kiislamu na uongozi wa Wilaya, pamoja na mataifa yote ya Kiislamu na wapigania uhuru duniani, kujitokeza kwa nguvu na kwa umoja katika matembezi ya Siku ya Quds Duniani.

Katika taarifa hiyo, amesisitiza kuwa; Siku ya Quds ya mwaka huu ni tofauti na miaka mingine, kwa sababu inakuja katika kipindi muhimu na cha mabadiliko makubwa ya kihistoria nchini Iran, katika eneo la Mashariki ya Kati na duniani kwa ujumla, sambamba na vita ya Ramadhani inayoamua hatima ya mambo. Hivyo, mwaka huu inapaswa kugeuka kuwa jukwaa kubwa na pana la kihistoria.

Ifuatayo ni nakala kamili ya taarifa hiyo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwenye kuwavunja madhalimu, kuwaangamiza waonevu na kuwafikia wale wanaokimbia.

Salamu na rehema zimfikie Mtume Mkuu (s.a.w.w.), Maimamu waongofu (a.s.) na Imam wa Zama (a.f.). Kwa mara nyingine tena, ninatoa pongezi na rambirambi kufuatia kuuawa kishahidi mashahidi wetu wapendwa miongoni mwa wananchi na vikosi vya ulinzi na usalama, hususan wanafunzi mashahidi, na zaidi ya yote, kuuawa kishahidi Imam wetu mpendwa, Imam Khamenei (r.a.).

Aidha, ninakumbusha umuhimu wa kuendelea wananchi kujitokeza kwa umoja na mshikamano katika medani mbalimbali, hususan katika Siku ya Quds Duniani.

Siku ya Quds ni urithi ulioachwa na Imam Khomeini (r.a.) na Imam Shahidi (r.a.). Wananchi wa Iran wenye msimamo thabiti, Umma wa Kiislamu na wapigania uhuru duniani wamekuwa wakiadhimisha siku hii kila mwaka na kuonesha uwepo wao wenye nguvu unaozivunja njama za maadui.

Hata hivyo, Siku ya Quds ya mwaka huu ni tofauti, kwa sababu inakuja katika kipindi muhimu na cha mabadiliko makubwa ya kihistoria nchini Iran, katika eneo la Mashariki ya Kati na duniani kwa ujumla, sambamba na vita ya Ramadhani inayoamua hatima ya mambo.

Wananchi mashujaa na wenye msimamo thabiti wa Iran wameugeuza mwezi mzima wa Ramadhani wa mwaka huu kuwa Siku ya Quds. Hata hivyo, ni muhimu kwamba Siku ya Quds ya mwaka huu igeuke kuwa jukwaa kubwa na pana la kihistoria.

Uwepo wa wananchi wetu wapendwa kwa namna ya kuvutia na yenye heshima katika kutetea Uislamu, Iran na Mapinduzi ya Kiislamu, pamoja na kufanya upya ahadi yao kwa Imam Khamenei Shahidi (r.a.), unapaswa kudhihirika kwa uwazi zaidi.

Vilevile, wanapaswa kuonesha utii na utiifu wao thabiti kwa kiongozi mpya na mtukufu, Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei, pamoja na kuviunga mkono vikosi vya ulinzi na usalama, wanajeshi wa Uislamu, wanachama wa Basij wenye thamani kubwa, walinzi wa usalama na Muqawama wa nchi.

Ninatoa shukrani na pongezi kwa wananchi wote, wanawake, wanaume na vijana wenye heshima, ambao katika mwezi mtukufu wa Ramadhani na katika medani hii ya kihistoria ya mapambano kati ya Uislamu na ukafiri, wamesimama kidete kwa kujitoa mhanga mbele ya njama tata za adui Mmarekani na Mzayuni, na wameonesha ushujaa uliowashangaza wengi. Vilevile, ninatoa pongezi na heshima kwa Muqawama wa ajabu na wa kushangaza uliooneshwa na vikosi vya ulinzi na usalama.

Aidha, ninatoa shukrani na pongezi kwa Maraji' wakuu wa kidini, wanazuoni, vituo na taasisi za kitamaduni na Hawza, pamoja na wanazuoni wote wa dini na wahubiri watukufu, na wasomi katika maeneo yote ya nchi. Ninathamini ushirikiano wao na wananchi katika medani zote, misikitini na katika shughuli mbalimbali, pamoja na juhudi na mapambano yao katika nyanja ya tablighi (uenezaji na ufafanuzi wa mafundisho ya dini) na Jihadi ya Ufafanuzi.

Ninawaomba wote waendelee kusimama imara, kwa umakini na ujasiri, katika mstari wa kujitokeza kwenye medani na kutekeleza Jihadi ya Ufafanuzi, hususan katika Siku ya Quds, hadi mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhani na kipindi chote cha mapumziko ya sikukuu za Nowruz. Bila shaka, kwa neema na msaada wa Mwenyezi Mungu, uwepo huu wa umoja na ushujaa wa taifa letu kubwa ni kitovu cha msingi na chemchemi inayobubujika ya nguvu za wananchi na mamlaka imara ya kitaifa na Kiislamu katika ulimwengu wa sasa.

Uwepo huu utaendelea kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, kwa baraka za maelekezo na uangalizi wa Mtukufu Waliyul-Asr (a.f.), na kwa baraka za damu safi za mashahidi, Inshaallah.

Tunazisalimia roho takatifu za mashahidi wote wenye heshima na fahari, Imam Mkuu (r.a.) na Imam Shahidi (r.a.).

Ayatullah Alireza Arafi
Mkuu wa Hawza Nchini Iran.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha